Tor (kama miundo ya sasa ya vitendo vya kutojulikana) inasindwa pale mshambuliaji anaweza kuona mwisho wote wa njia ya mawasiliano.
Kwa mfano, mshambuliaji anayeendesha au anaona Tor relay uliyochagua kuingia kwenye mtandao, pia anaendesha na kuona tovuti unazotembelea.
Kwa tatizo hili, jumuiya ya tafiti wanajua hakuna sheria madhubuti iliyotengenezwa amabayo inaweza kumzuia mshambuliaji kuhusianisha taarifa za kiwango na muda kwa pande hizo mbili.
Hivyo, tunatakiwa kufanya nini?
Tuseme mshambuliaji anaendesha au anachunguza , njia za relay C.
Tuseme kuna jumla ya relay N.
Kama utachagua njia mpya za kuingia na kutoka kila wakati unapotumia mtandao, mshambuliaji anaweza akahusianisha upekuzi wote ulioufanya ndani ya muda huo (c/n)2.
Kwa ufupi, kwa watumiaji wengi, ni vibaya kama hufuatiliwa kila wakati: wanataka kufanya kitu bila ya mshambuliaji kutambua, na mshambuliaji akitambua mara moja ni mbaya kama ambavyo mshambuliaji akitambua zaidi.
Hivyo, kuchagua njia nyingi za kuingilia na kutokea bila mpangilio haimpi mtumiaji nafasi ya kujiondoa kwenye maelezo mafupi kwa aina hii ya mshambuliaji.
Njia ya utatuzi ni "kuweka ulinzi": kila mtumiaji wa Tor anachagua njia chache bila mpangilio kutumia pointi za kuingilia na kutumia njia hizo pekee kwa mara yao ya kwanza katika hop.
Kama vifaa vyote havijaendeshwa au kuchunguzwa , mshambuliaji hawezi kushinda kamwe na mtumiaji atakua salama.
Kama vifaa vyote vinachunguzwa na kuendeshwa na mshambuliaji, huyo mshambuliaji anaona sehemu kubwa ya upekuzi wa watumiaji lakini bado mtumiaji hawi na maelezo zaidi ya awali.
Hivyo, mtumaji ana baadhi ya nafasi (katika agizo la(n-c)/n)la kuzuia maelezo mafupi, japokuwa hazikuwepo kabla.
Unaweza kusoma zaidi kwenye Uchambuzi wa uharibifu wa itifaki usiojulikana, kutetea mawasiliano yasiojulikana dhidi ya mashambulizi ya ukataji magaogo, na hususani kutafuta seva zilizofichwa.
Kuzuia node zako za kuingia vilevile inaweza kusaidia dhidi ya washambuliaji ambao wanataka kutumia nodes zako kirahisi na kuhesabu kwa urahisi anwani zote za IP za watumiaji wa Tor.
(Japokuwa hawawezi wakajifunza ni maeneo gani watumiaji wanazungumza nao, bado wanaweza wakafanya vitu vibaya kwa orodha hiyo ya watumiaji.)
Hata hivyo, kipengele hicho hakitakuwa na uhumimu hadi tutakapohamia kwenye saraka guard.