Nawezaje kujua kama natumia onion service za v2 au v3?
Unaweza kutambua teleo la 3 la anwani ya onion kwa urefu wa herufi 56, mfano. Tor Project's v2 address:http://expyuzz4wqqyqhjn.onion/
, and Tor Project's v3 address: http://2gzyxa5ihm7nsggfxnu52rck2vv4rvmdlkiu3zzui5du4xyclen53wid.onion/
Ikiwa wewe ni msimamizi wa onion service, unapaswa kusasisha toleo la 3 la onion service haraka iwezekanavyo.
Ikiwa wewe ni mtumiaji, tafadhari hakikisha umesasisha alamisho yako katika anwani ya tovuti toleo la 3 la onion.
Rekodi yako ya matukio ni ipi kwenye v2?
Mnamo September 2020, Tor walianza kutoa onyo kwa waendeshaji na watumiaji wa onion service kuwa toleo la 2 litaacha kutumika na toleo la zamani la 0.4.6.
Tor Browser ilianza kutoa onyo kwa watumiaji wake June, 2021.
MnamoJuly 2021, toleo la 0.4.6 la Tor haitatumia tena toleo la 2 na usaidizi utaondolewa katika msingi wa msimbo.
Mnamo October 2021, Tutatoa toleo jipya la watumiaji wa Tor toleo lililo imara kwa safu zote ambazo zitaondoa uwezo wa toleo la 2.
Unaweza kusoma zaidi katika machapisho ya blog ya Tor project's Onion Service version 2 deprecation timeline.
Ninaweza kuendelea kutumia anwani za onion zangu za v2? Ninaweza kupata onion zangu za v2 baada ya mwezi wa tisa? Hii ni mabadiliko ya nyuma yasiyolingana?
Anwani za toleo la 2 la onion hazipo salama kimsingi, Kama una toleo la 2 la onion, tunapendekeza uache kulitumia.
Haya ni mabadiliko ya awali yasiyoendana: Toleo la 2 la onion services haitapatika baada ya September 2021.
Ni pendekezo gani kwa watengenezaji programu ili kuhamisha? Vidokezo vyovyote vya namna ya kusambaza anwani mpya za V3 kwa watu?
Katika torrc, kutengeneza anwani ya toleo la 3, utahitaji tu kuanzisha huduma mpya kama ulivyofanya tu katika huduma ya toleo la 2, kupitia mistari hii miwili:
HiddenServiceDir /full/path/to/your/new/v3/directory/
HiddenServicePort <virtual port> <target-address>:<target-port>
Toleo lililozoeleka kwa sasa limepangiliwa kuwa la 3 kwa hivyo hupaswi kuweka wazi.
Anzisha tena tor, na angalia katika saraka yako kwa ajili ya anwani mpya.
Ikiwa unataka kuendelea kutumia huduma yako ya toleo la 2 hadi pale itakapoacha kutoa njia ya mpito kwa watumiaji wako, ongeza mstari huu ili kusanidi huduma yako ya toleo la 2 iliyozuiliwa:
HiddenServiceVersion 2
Hii itakuruhusu kutambua faili lako ulilolisanidi ni lipi katika toleo lipi.
Ikiwa una Onion-Location sanikisha tovuti yako, unahitaji kupangilia kichwa cha habari na toleo lako la 3 jipya la anwani.
Kwa nyaraka ya kiufundi kuhusu kutumia onion services, tafadhari soma kurasa ya Onion Services katika Portal yetu ya kijamii.
Sijaona tangazo, ninaweza kupata muda zaidi wa kuhama?
Hapana, mawasiliano ya toleo la 2 yataanza kushindwa sasa hivi, kuanza polepole, kisha ghafla. Ni wakati wa kuyaondoka.
Huduma zitaanza kushindwa kufika mwezi wa tisa, au tayari kabla?
Tayari, alama za utangulizi hazipo katika Tor 0.4.6 kabisa, hivyo haziwezi kupatikana kama waendesha relay watasasisha.
Wasimamizi wa tovuti, ninaweza kurudia kuwaongoza watumiaji kutoka kwenye onion ya v2 hadi v3?
Ndio, Itafanya kazi hadi toleo la 2 la onion address lisipopatikana.
Unaweza kuhitaji kuwahimiza watumiaji kusasisha amalisho zao.
Onion service za v3 inakwenda kusaidia kupunguza matatizo ya DDoS?
Ndio, tunaendelea kushughulikia katika kuboresha usalama wa onion services.
Baadhi ya kazi tulizonazo katika mipango yetu ni ESTABLISH_INTRO Cell DoS Defense Extension, Res tokens: Anonymous Credentials for Onion Service DoS Resilience, na A First Take at PoW Over Introduction Circuits.
Kwa muhtasari kuhusu mapendekezo haya, soma chapisho la blog Namna ya kuzuia kushindwa kwa onion (za huduma).